kimataifa

AUBA AMPASUA KICHWA ARTETA

admin February 1, 2021 6:47 am


 PIERRE Emerick Aubameyang, nahodha wa kikosi cha Arsenal kwa sasa bado yupo karantini na haijulikani atarejea lini uwanjani jambo ambalo linampasua kichwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Mikel Arteta.

Raia huyo wa Gabon alitarajiwa kurejea uwanjani kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United uliokamilika kwa sare ya bila kufungana ila alikosekana ndani ya uwanja.

Auba amewekwa karantini baada ya kutoka kumjulia hali mamaye ikiwa ni kuchukua tahadhari dhidi ya janga la Corona ili kujua kwamba hajarudi na Corona.

Arteta amesema kuwa:”Alikuwa amekwenda kumuona mamaye ila kwa sasa yupo karantini hivyo tunapaswa kufuata taratibu na hatuwezi kumtumia kwa sasa,” .

MO SALAH ATUPIA MAWILI WAKATI TIMU YAKE IKISEPA NA POINTI TATU MBELE YA WEST HAM UNITED JEMBE JIPYA YANGA LAPEWA JEZI YA MAPINDUZI, MAZOEZI YAKE NOMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply