kimataifa

MO SALAH ATUPIA MAWILI WAKATI TIMU YAKE IKISEPA NA POINTI TATU MBELE YA WEST HAM UNITED

admin February 1, 2021 6:47 am


 WEST Ham United walikubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Liverpool, mchezo wa Ligi Kuu England usiku wa kuamkia Januari 31.

Mshambuliaji wa Liverpool, raia wa Misri Mohamed Salah alitupia mabao mawili dakika ya 57 na 68 na lile la tatu lilifungwa na Georginio Wijnaldum dakika ya 84.

West Ham United walipata bao la kufuta machozi kupitia kwa Craig Dawson aliyepachika bao hilo dakika ya 87.

Ushindi huo unaifanya Liverpool kupanda nafasi moja kutoka ile ya nne mpaka nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 40 ikiwa imecheza jumla ya mechi 21 na West Ham United inabaki nafasi ya tano ikiwa na pointi 35 na imecheza jumla ya mechi 21.


GOMES AWAKAZIA MAZEMBE, ATAJA SABABU ZA SARE NA KUSEPA NA KOMBE AUBA AMPASUA KICHWA ARTETA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply