Home Simba SC SIMBA KUTINGA BUNGENI KUPEWA BARAKA ZA LIGI YA MABINGWA

SIMBA KUTINGA BUNGENI KUPEWA BARAKA ZA LIGI YA MABINGWA


 UONGOZI wa Klabu ya Simba umesema kuwa kesho timu hiyo itapata nafasi ya kuingia bungeni kwa ajili ya kupewa baraka na wawakilishi wa Tanzania kwa ajili ya mechi zao za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Inanolewa kwa sasa na Didier Gomes raia wa Ufaransa ambaye alichukua mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye alibwaga manyanga Januari 7 ndani ya Simba.

Kwa sasa Sven yupo zake ndani ya FAR Rabat ya Morocco akiwa ni kocha mkuu wa timu hiyo na amesaini dili la miaka miwili. 

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema:” Kikosi kinaanza maandalizi kwa ajili ya ligi na kesho kinatarajia kuondoka Bongo asubuhi.

“Wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja baada ya kumaliza mchezo wa Simba Super Cup hivyo wanarejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za mbele ikiwa ni zile za ligi na Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tutaondoka asubuhi Jumatano ili kwenda Dodoma kwa ajili ya mchezo wetu wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji FC ambao utachezwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma, lakini pia tutapata nafasi ya kwenda bungeni Februari 3. 

“Bungeni tutakwenda kupata baraka za Wabunge wetu hasa ukizingatia kwamba tunakwenda kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Februari 5 baada ya mchezo wetu tutarudi Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu wa ligi dhidi ya Azam FC,” amesema.

Mabingwa hao wa Simba Super Cup mchezo wao wa mwisho ilikuwa ni Januari 31 ambapo walicheza na TP Mazembe.

Dakika 90 zilikamilika kwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Mkapa ambapo kikosi cha Gomes kilibadilika tofauti na kile ambacho kilishinda mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal, Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mchezo wa kwanza kiungo mshambuliaji Miraji Athuman alianza benchi ila kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe alianza kikosi cha kwanza.

SOMA NA HII  SIMBA WATIA MKONO KWENYE MCHEZO WA 'BASKETBALL'...JAMBO LAO HILI HAPA...