UONGOZI wa Klabu ya Yanga umewashusha presha mashabiki wake kuhusu suala la kupigwa pini na FIFA kufanya usajili kwa muda wa miaka mitatu.
Imeelezwa kuwa Yanga imefungiwa na FIFA kufanya usajili kwa kuwa haijalipa deni la mchezaji wao wa zamani Amiss Tambwe ambalo ni la mshahara wake pamoja na fedha za usajili.
Kwa mujibu wa Tambwe amesema kuwa amepewa taarifa na mwanasheria wake ambayo imeeleza kuwa Yanga wamezuiwa kufanya usajili kwa muda wa misimu mitatu.
“Nimepewa taarifa na mwanasheria wangu kwamba Yanga haitapaswa kusajili kwa muda wa miaka mitatu yaani kwenye dirisha dogo na dirisha kubwa la usajili hiyo ni taarifa ambayo nimepewa.
“Mimi sina tatizo na Yanga ila taarifa ninapewa na mwanasheria wangu na hilo ndilo ambalo ninalijua kwa sasa.
Kuhusu hilo Ofisa Uhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Anthonio Nugaz amesema:- “Deni la Tambwe Milioni 41 anazodai zilitalipwa ndani ya muda mfupi na wana Yanga wasiwe na hofu yoyote.
“Hiyo pesa inalipwa na usajili kwa Yanga utaendelea kama kawaida.Hiyo ni pesa kidogo kwa Yanga,tumepokea maamuzi ya FIFA na Sisi tunalipa wakati wowote na kila kitu kitakwenda sawa na tutaendelea kusajili wachezaji,” .
Yanga imeweka kambi Kigamboni na imekamilisha usajili wa nyota watatu kwenye dirisha dogo ambao ni Fiston Abdulazack, Said Ntibanzokiza na Dickson Job.