Simba SC

MSHAMBULIAJI WA SIMBA AMBAYE INATAJWA KAPORWA NA YANGA ATAJA ALIPO

admin August 2, 2021 9:43 pm

 NTOTA Peter Banda amesema kuwa kwa sasa yupo Msumbiji na awali ilipaswa aje na timu ya Big Bullets Bongo ila mambo yalikwenda tofauti.


Big Bullets ambayo ni timu yake ipo Tanzania ikishiriki mashindano ya Kagame na Agosti Mosi iligawana pointi mojamoja na Yanga baada ya kupata sare ya kufungana bao 1-1.


Habari zinaeleza kuwa Simba wapo kwenye hesabu za kuinasa saini yake huku Yanga nao wakitajwa kuingilia kati dili hilo.


Jana alikuwa anapewa nafasi ya kutambulishwa ndani ya Simba ila mambo yalikwenda tofauti na hakuweza kutambulishwa.


 Kwa sasa inaelezwa kuwa alipelekwa Kigamboni kumalizana na mabosi wa Yanga ambao waliamua kuwazunguka watani zao Simba ambao walikuwa wanapewa nafasi ya kumpa dili nyota huyo.


Banda mwenyewe amesema kuwa yupo Malawi ila aliweka wazi kuwa alikuwa anawasiliana na viongozi wa Simba ambao walikuwa wanahitaji kumpa ofa mshambuliaji.

Kuhusu usajili wa Yanga, Ofisa Habari wa timu hiyo Hassan Bumbuli alisema kuwa wanakwenda kimyakimya na wachezaji watakaokamilisha madili watatambulishwa.

HARRY KANE ANATAKA KUONDOKA SPURS NYOTA WA U 23 KELVIN HONGERA KWA KUONGEZA MWAKA MMOJA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply