kimataifa

HARRY KANE ANATAKA KUONDOKA SPURS

admin August 2, 2021 9:43 pm


HARRY Kane nyota wa timu ya Tottenham amewaambia mabosi wake kwamba hayupo tayari kuwa ndani ya timu hiyo kwa msimu ujao jambo ambalo linamfanya ahitaji kupata changamoto mpya.

Nyota huyo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya England kwa muda mrefu amekuwa akitajwa kuingia kwenye rada za Manchester City, Chelsea na Arsenal ambao wanahitaji saini yake.

Kwa mujibu wa Sky Sports ripoti zimeeleza kuwa Kane amewaambia mabosi wa timu yake kwamba kwa msimu huu anahitaji kuondoka Spurs jambo ambalo linamfanya afungue njia kwenye timu nyingine ambazo zinamuhitaji.  

Mwenyekiti wa Man City, Khaldoon Al Mubarak hivi karibuni alibainisha kwamba wanahitaji kusajili kikosi bora ambacho kitakuwa na ushindani zaidi jambo ambalo linatoa nafasi kwao kuweza kumpata Kane ilikuwa ni baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Tunahitaji kuwa kwenye ushindani na utayari kwa ajili ya msimu ujao. Kwa msimu huu tutaimarisha kikosi kwa kuleta wachezaji bora na wenye uwezo mkubwa,” 

MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE MSHAMBULIAJI WA SIMBA AMBAYE INATAJWA KAPORWA NA YANGA ATAJA ALIPO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply