Simba SC

MZEE WA KUKERA MORRISON AAHIDI MAKUBWA NDANI YA TIMU YAKE

admin February 5, 2021 11:47 pm

 


BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji ndani ya Klabu ya Simba amesema kuwa furaha yake ni kuona malengo ya timu hiyo yanatimia hivyo ataendelea kupambana.


Hivi karibuni ilielezwa kuwa nyota huyo raia wa Ghana hawezi kucheza mechi za ushindani atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita kwa kuwa anasumbuliwa na Hernia pamoja na majeraha ya muda mrefu.


Taarifa hiyo ilipingwa na Uongozi wa Simba ukiongozwa na Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez pamoja na Ofisa Habari, Haji Manara. 


Barbara aliweka wazi kuwa Morrison ni mzima na ni mali ya Simba huku Manara akisisitiza kwamba Morrison atacheza Simba Super Cup pamoja na mashindano mengine bila mashaka.


Kwenye Simba Super Cup,  alicheza mechi zote mbili mbele ya Al Hilal alifunga mabao mawili yaliyompa tuzo ya mfungaji bora na alicheza pia mbele ya TP Mazembe.  Februari 4 alicheza mbele Dodoma Jiji ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara na alifunga bao moja wakati timu hiyo ikishinda mabao 2-1.


Morrison ambaye amebatizwa jina la mzee wa kukera amesema:”Ninafurahi kuwa ndani ya Simba na malengo ni kuona timu inapata matokeo na kufikia malengo hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti,”.

HESABU ZA MTIBWA SUGAR MZUNGUKO WA PILI ZIMECHORWA NAMNA HII MTAMBO WA MABAO YANGA WATOA KAULI YA MATUMAINI KISA FISTON

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply