Simba SC

KOCHA SIMBA AFUNGUKIA USHINDI DHIDI YA AS VITA

admin February 13, 2021 10:47 am

 


KOCHA mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes Da Rosa amefunguka kuwa ushindi walioupata dhidi ya AS Vita kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ni mwanzo mzuri kwao kufanya vizuri zaidi katika michuano hiyo mwaka huu.

Simba jana usiku iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao AS Vita, katika mchezo wa kwanza wa kundi A uliofanyika katika Stade Des Martyrs, Kinshasa nchini Congo.

Ushindi huo umeifanya Simba kuongoza msimamo wa kundi A wakiwa na pointi zao tatu na faida ya bao moja, ambapo wanasubiri kuona matokeo ya mchezo wa Al Ahly na Al Merrikh.

Akizungumzia furaha yao baada ya ushindi huo dhidi ya AS Vita Gomes amesema: “Tumefurahi sana na tumeridhishwa sababu tulicheza vizuri na matokeo ni mazuri.

“Kwa Simba matokeo haya yatakuwa na faida mbeleni katika hatua hii ya makundi na katika kutimiza adhima yetu ya kufanya vizuri,”

NYOTA HAWA WA YANGA KUIKOSA MBEYA CITY LEO FISTON: YANGA SC TULIENI, NITAFUNGA TU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply