LICHA ya Uongozi wa Yanga kupitia kwa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hersi Said ambaye ni Injinia akiwa ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM kukabidhiwa hesabu za fedha ambazo Yanga inadaiwa na Amissi Tambwe bado hajalipwa.
Staa huyo wa Burundi aliyekipiga ndani ya Yanga amesema kuwa bado hajalipwa fedha zake ambazo ni milioni 41 baada ya kufungua kesi FIfa kwa kile alichoeleza kuwa hakulipwa stahiki zake pamoja na fedha za usajili.
Fifa iliiamuru Yanga kulipa mkwanja huo kwa Tambwe ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya posho na mshahara wake.
Tambwe amesema:-“Tumekamilisha kuwasilisha hesabu kwa mabosi ila mpaka sasa hakuna ujumbe niliopata kwamba fedha zimeingia ama na sielewi Yanga wamekwama wapi?.
“Sikuwa na lengo la kufika Fifa na wala sijafulia kama ambavyo wengi wanaeleza ukweli ni kwamba ninadai jasho langu na nilafanya kazi nikiwa ndani ya Yanga.
“Kwa kuwa jukumu lao nilitimiza kwa wakati hivyo nao ni jukumu lao kunilipa, ikiwa watashindwa sijui nini kitafuata kwani hilo jukumu ni lao na sio mimi tena,”.
Hivi karibuni, Injinia Hersi alinukuliwa akisema kuwa watashugulikia suala hilo na kulipa kwa wakati.