Home Ligi Kuu KAGERA SUGAR YATUMA SALAMU YANGA

KAGERA SUGAR YATUMA SALAMU YANGA


MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga kwa kuwa wanazitaka poiti tatu.

Kagera Sugar, Februari 11 ilikamilisha kwa kupata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Gwambina FC, Uwanja wa Kaitaba inakutana na Yanga iliyotoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Februari 17 Uwanja wa Mkapa unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa mchezo wao wa mzunguko wa kwanza Kagera Sugar ilipoteza pointi tatu kwa kufungwa bao 1-0, Uwanja wa Kaitaba.

Akizungumza na Saleh Jembe Maxime amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zote za mzunguko wa kwanza na wanaamini kwamba watapata pointi tatu muhimu.

“Kwenye mechi zetu zote ndani ya uwanja  tumejipanga kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu hivyo mchezo wetu ujao dhidi ya Yanga nao ni sehemu ya mchezo, tutaingia kwa kuwaheshimu ila tunazihitaji pointi tatu.

“Mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti kwani ushindani ni mkubwa na wapinzani wetu nao sisi tunawaheshimu hivyo,”.

Kwenye msimamo wa ligi, Kagera Sugar ipo nafasi ya 10 na pointi 23 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya kwanza na pointi 45 zote zimecheza jumla ya mechi 19.

SOMA NA HII  KISA CAF.....SIMBA, YANGA ZAPIGWA 'KALENDA' TFF......