NDANI ya Ligi Kuu England, Mohamed Salah ni kinara wa utupiaji akiwa ametupia jumla ya mabao 17 msimu wa 2020/21, timu yake ya Liverpool ipo nafasi ya nne.
Raia huyo wa Misri anaamini kwamba bado timu yake hiyo ina nafasi ya kufanya vizuri na kuweza kutwaa taji hilo tena kwa msimu huu licha ya kuwa kwenye mwendo wa kusuasua hivi karibuni.
Inapambana kutetea taji Ligi Kuu England ililotwaa msimu uliopita wa 2019/20 chini ya Jurgen Klopp.
Anafuatiwa kwa ukaribu na nyota wa Manchester United, Bruno Fernandes ambaye amefunga jumla ya mabao 14 na timu yake ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 46.
Kinara wao ni Manchester City ya Pep Guardiola ikiwa na pointi 53 baada ya kucheza jumla ya mechi 23.
Salah amesema:”Wengi wapo nyuma yetu wanapenda kuona tunafanya vizuri hilo lipo wazi na tunaamini kwamba tunaweza kufikia malengo hayo na tutafanya vizuri katika kutetea taji,”.