Home Yanga SC BAADA YA KUGAWANA POINTI MOJAMOJA, YANGA WATOA SABABU

BAADA YA KUGAWANA POINTI MOJAMOJA, YANGA WATOA SABABU


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa matokeo ambayo wameyapata leo ndani ya uwanja ni sehemu ya mchezo na imetokana na wachezaji wao kushindwa kutumia nafasi ambazo walizipata kipindi cha kwanza na cha pili.

Ikiwa nyumbani, Uwanja wa Mkapa ilikubali sare ya kufungana mabao 3-3 mbele ya Kagera Sugar na kugawana pointi mojamoja.

Ni Kagera Sugar walianza kufungua akaunti ya mabao dakika ya 10 kupitia kwa Peter Mwalanzi na lilidumu kwa muda wa dakika nne ambapo Yanga waliweka mzani sawa dakika ya 14 kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Tuisila Kisinda.

Hasan Mwaterema alitumia dakika 9 kuandika bao la pili kwa Kagera Sugar na lilidumu dakika 6 kwa Deus Kaseke kuweka usawa dakika ya 29.

Ikiwa kwenye dakika zile za nyongeza kukamilisha dakika 45, nyota wa Kagera Sugar, Yusuph Mhilu alipachika bao la tatu dakika ya 45+ 1 na kuwafanya Yanga waende mapumziko wakiwa nyuma kwa bao moja.

Kipidi cha pili Yanga walikuja kwa kasi na kupachika bao la usawa dakika ya 60 kupitia kwa Mukoko Tonombe kwa shuti kali akiwa nje ya 18.

Mpaka dakika 90 zinakamilika ubao ulikuwa unasoma 3-3 na timu zote zimegawana pointi mojamoja.

Kaze amesema:”Ni makosa yetu kushindwa kukamilisha mchezo ndani ya kipindi cha kwanza na cha pili kwa kuwa tulipata nafasi tukashindwa kuzitumia hivyo hakuna wa kumlaumu katika hili,”. 

Mecky Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa wametoa burudani na mabao wamefunga.

SOMA NA HII  YANGA WAFUNGUKA SABABU YA NYOTA WAO WATATU KUUKOSA MCHEZO WA J/PILI..WAFUNGIWA NA CAF