Ligi Kuu

KMC YAZITAKA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR

admin February 19, 2021 12:47 pm


Mara baada ya kuibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Mwadui FC, Timu ya KMC FC kwa mara nyingine itashuka dimbani kesho kumenyana na Kagera Sugar katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.


Katika mchezo huo, KMC ambao ni wenyeji dhidi wapinzani wao Kagera Sugar, utachezwa saa 8:00 mchana ambapo tayari maandalizi ya mwiso yamefanyika na kwamba wachezaji wote wapo kwenye morali nzuri kuelekea kwenye mtanange huo.


Timu ya KMC ambayo ipo chini ya kocha mkuu John Simkoko inahitaji ushindi katika mchezo huo ilikuweka ilikuweza kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara.


 “ Tunahitaji kushinda mchezo wetu wa kesho, ushindi ni mkakati wetu wa kwanza, tunajua duru hii ni ngumu kwasababu kila timu inahitaji alama tatu muhimu, kikubwa tunaendelea kujituma katika maandalizi yetu kila mchezo kwetu ni fainali lengo ni kuhakikisha kwamba kwenye mchezo huo tunakwenda kupata alama tatu.


Hadi sasa KMC ipo kwenye nafasi ya sita ikiwa na alama 28 na kucheza michezo 20, mbapo Februali 16 ilipata ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya mwadui, mchezo uliopigwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.


Imetolewa na Christina Mwagala


Afisa Habari na Mahusiano wa Timu ya KMC

SIMBA WAFICHUA MBINU YA KUWAMALIZA WAARABU KWA MKAPA SIMBA WAJA NA POINTI OF NO RETURN KUWAKABILI WAARABU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply