Ligi Kuu

POLISI TANZANIA HESABU ZAO MZUNGUKO WA PILI HIZI HAPA

admin February 19, 2021 2:47 pm


UONGOZI wa Polisi Tanzania umesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mzunguko wa pili ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Polisi Tanzania inanolewa na Kocha Mkuu, Malale Hamsini ipo nafasi ya 9 ikiwa imecheza jumla ya mechi 19 na imekusanya jumla ya pointi 24.

Mchezo wake uliopita wa ligi ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.

 Frank Lukwaro, Ofisa Habari wa Polisi Tanzania amesema kuwa wanatambua kwamba kila timu inahitaji pointi tatu hivyo nao watapambana kupata matokeo chanya.

“Mzunguko wa pili ni muda wa kila timu kupambana kupata pointi tatu kwa kuwa ni muda wa lala salama hivyo hakuna mechi ambayo itakuwa nyepesi.

“Tupo tayari kwa ajili mechi zetu za mzunguko wa pili na tutafanya vema hivyo mashabiki watupe sapoti kwenye mechi zetu,” amesema. 

DK MSOLLA ANAKUMBUSHWA MAKOSA WAKATI AKIWA PEMBENI YA USUKANI…. KOCHA SPURS ANATAJWA KUWEKWA KWENYE HESABU ZA KUFUTWA, ATOA KAULI YA KISHUJAA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply