UONGOZI wa Simba kupitia kwa Ofisa Habari wao, umewajibu kimtindo watani zao wa jadi Yanga kuhusu suala lao la kusema kwamba wanaweza kujiondoa kwenye Ligi Kuu Bara.
Leo Februari 19, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa ikiwa waamuzi watashindwa kuwatendea haki kesho kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar wanaweza kujiondoa kushiriki ligi.
Yanga inoangoza ligi ikiwa na pointi 46 baada ya kucheza jumla ya mechi 20 inafuatiwa na Simba iliyo nafasi ya pili na pointi zao ni 42 ikiwa imecheza jumla ya mechi 18.
Mwakalebela amesema kuwa kwa namna ambavyo mazingira yapo inaonekana kama kuna bingwa ambaye amepangwa jambo ambalo linawafanya wawe wananyimwa haki zao wanapokuwa ndani ya uwanja.
“Kwa namna mwendo unavyokwenda inaonekana kwamba kama kuna bingwa ambaye amepangwa, hivyo ikiwa kesho kwenye mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar, waamuzi watashindwa kututendea haki basi tunaweza kujiondoa kushiriki ligi,” ,
Haji Manara akizungumza naye leo Februari 19 amesema kuwa kuna wanaotishia kususa kushiriki ligi kama wataamua wafanya hivyo.
“Mimi nazungumzia habari za Simba na Al Ahly, sizungumzii habari ya kulalamikalalamika, si uamuzi tu huu, kususa, unasusa, susa nasema susa, unasema hayo baada ya kuona wanaume wanakuja namna hii wanaanza kutafutana.
“Unamtisha nani, hii yote unawatisha waamuzi hii yote unayasema wakati huu mbona ulipokuwa unaongoza ligi ulikuwa husemi haya, haya yote sasa kila siku Morrison akishinda inakuwa shida, basi kesho tutamwambia Morrison asifunge,”.