KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina leo Februari 22 kitawakaribisha Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Ikiwa Azam FC ipo nafasi ya tatu na pointi 36 baada ya kucheza mechi 20 inakutana na Prisons iliyo nafasi ya 8 na pointi zake 25.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Azam FC ilishinda bao 1-0 lilipachikwa na Prince Dube hivyo leo kazi itakuwa moja kwa Azam FC kulinda rekodi yao huku Prisons wakiwa na hesabu za kutibua hesabu za Azam FC.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kikosi kipo tayari na wachezaji wana morali kubwa ya kupambana ili kupata ushindi ndani ya uwanja.
“Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Prisons, tunawaheshimu wapinzani wetu ila nasi pia tupo tayari ili kupata matokeo chanya ndani ya uwanja,”.