Simba SC

NAHODHA WA AL AHLY ATUMA UJUMBE SIMBA

admin February 22, 2021 6:47 pm

 

NAHODHA wa Al Ahly, Aiman Ashraf amesema kuwa wamekuja Dar kwa ajili ya kupata ushindi mbele ya wapinzani wao Simba.


Kesho, Februari 23 Al Ahly itakaribishwa na Simba, saa 10:00 kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya makundi.

Mchezo huo unatarajiwa kuchukua jumla ya mashabiki 30,000 kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika,(Caf) kwa ajili ya kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Nahodha huyo amesema:”Lengo letu kubwa ni kutwaa ubingwa na tunajua tunacheza na timu kubwa hivyo hatutadharau jambo lolote.

“Kuhusu muda wa mechi hauwezi kuwa kikwazo kwetu. Tumekuja kupambana tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo hivyo tutaingia kwa tahadhari na tunawaheshimu wapinzani,”.


TONOMBE MUKOKO YUPO FITI KWA AJILI YA MECHI ZIJAZO MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply