Simba SC

WAARABU WA SIMBA WAUKAGUA UWANJA WA MKAPA,NGUVU YAO IPO KWA MAWINGA

admin February 22, 2021 12:47 pm


 PITSO Mosimane, Kocha Mkuu wa Al Ahly, Pitso Mosimane nguvu yake kubwa kwenye kutafuta ushindi inategemea upande wa mawinga huku washambuliaji wakimaliza kazi.

Leo Februari 22 Waarabu hao wa Misri wameukagua Uwanja wa Mkapa ambao utatumika kesho kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya makundi.

Kesho Februari 23 itashuka kwenye uwanja huo kusaka ushindi mbele ya Simba majira ya saa 10:00 jioni.

Vita kubwa itakuwa kwa upande wa eneo la kati ambalo Simba imekuwa ikipenda kutumia kwenye kusaka ushindi ndani ya uwanja.

Mosimane amesema kuwa anatambua utakuwa mchezo mgumu ila anawatambua wapinzani wake hawatampa shida atapata matokeo.

Didier Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anaamini kwamba watakutana na ushindani mkubwa ila watapambana kusaka ushindi.

“Mchezo utakuwa mgumu hilo lipo wazi ila tutapambana kusaka ushindi. Matokeo mazuri mbele ya Biashara United na AS Vita yametupa nguvu ya kuwa kwenye morali ya kusaka ushindi,”.

SIMBA YATAJA MASHINE YAO YA KAZI ITAKAYOWAPA USHINDI MBELE YA AL AHLY TAMBWE:BADO SIJALIPWA BADO NA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply