Home Azam FC KOCHA AZAM AMPA KAZI MAALUM MUUAJI WA SIMBA

KOCHA AZAM AMPA KAZI MAALUM MUUAJI WA SIMBA


KOCHA msaidizi wa klabu ya Azam, Vivier Bahati amesema kuwa watalazimika kuwapa kazi maalum mawinga wao wakiongozwa na muuaji wa Simba, Idd Selemani Nado katika michezo ijayo ili kumaliza changamoto ya kukosa ushindi wanayopitia.

Nado alikuwa mhimili mkubwa wa Azam katika mchezo wa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba Februari 7, mwaka huu akifunga bao moja na kuasisti bao la pili lililofungwa na Ayoub Lyanga.

Azam Jumatatu iliyopita ililazimishwa suluhu na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons, mchezo uliopigwa katika dimba la Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam. 

Suluhu katika mchezo wa juzi imeifanya Azam sasa kufikisha pointi 37 baada ya kucheza michezo 21 hivyo kusalia katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi.

Akizungumzia mchezo huo, kocha Bahati amesema: “Tumepata sare dhidi ya Prisons katika mchezo uliopita, ni matokeo ambayo hatukuyatarajia kwani tulijipanga vizuri kabla ya mchezo na pia tulionyesha kiwango kizuri.

“Lakini wapinzani wetu walitulazimisha kucheza mchezo wa fiziki kubwa na kugongana mara kwa mara, jambo lililotulazimisha kucheza nje ya mipango yetu.

“Lakini tayari tumekuja na suluhisho ambapo katika hali kama hiyo kwenye michezo ijayo, tutatumia zaidi mawinga kama Idd Nado na Ismail Aziz ‘Kader’ ili kuweza kutanua zaidi uwanja na kutengeneza nafasi kwa mipira ya chini,”

SOMA NA HII  BAADA YA KUTANGAZA KUACHANA NAYE...AZAM FC WAIBUKA NA HAYA MAPYA KUHUSU MUDATHIRI YAHYA...