KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen, leo Februari 26 ametangaza kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kitakachoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kuwania kufuzu Afcon.
Nyota 10 wameitwa kutoka kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu.
Hawa hapa wachezaji walioitwa na Poulsen:- Aishi Manula yeye ni kipa namba moja wa Simba
Shomari Kapombe yeye ni beki wa pembeni
Erasto Nyoni huyu ni kiraka ndani ya kikosi.
Kennedy Juma yeye ni beki wa kati.
Mohamed Hussein ‘Tshabalala’,beki wa pembeni.
Hassan Dilunga kiungo mshambuliaji.
Mzamiru Yassin kiungo mkabaji.
Said Ndemla kiungo mkabaji.
John Bocco yeye ni mshambuliaji
Jonas Mkude ni kiungo mkabaji