Simba SC

SAMATTA Sr :- HUYU MIQUISSONE HUYUU..!!

admin February 26, 2021 3:06 pm


BABA mzazi wa Mbwana Samatta, anayekipiga Uturuki kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Aston Villa ya England, ameshindwa kujizuia kwa Luis Miquissone wa Simba.

Mzee huyo anayejulikana kwa jina la Ally Pazi Samatta amesema Miqussone ni mchezaji hatari aliyetetemesha Misri kwa kiwango alichokionyesha timu yake ikicheza na Al Ahly.

Katika mchezo huo Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0, mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, jambo ambalo limewapa ujasiri mashabiki wa Msimbazi kutembea kifua mbele.

Mzee Samatta amesema Miquissone ameonyesha maana halisi ya timu kusajili wageni wanaokusudiwa kuleta changamoto ya ushindani.

“Kimo chake kifupi hakikuzuia kuburuza ngome ya ulinzi ya Al Ahly, haogopi kupita katikati yao, huo ni ujasiri wa aina yake,” amesema na ameongeza kuwa;

“Miquissone hakuugopa kabisa mchezo ndio maana alicheza kwa kujiamini, wanatakiwa wachezaji wote wawe hivyo naamini wanaweza wakafanya kitu hata ugenini,”amesema.

Amesema amefunga bao la maarifa ambalo hata Al Ahly limewavutia na kuanza kutamani huduma yake.

WANNE WA AZAM FC WAITWA KUUNDA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA JE ! HUU NDIO MWISHO WA MAPINDUZI BALAMA NDANI YA YANGA SC?

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply