Azam FC

WANNE WA AZAM FC WAITWA KUUNDA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA

admin February 26, 2021 2:47 pm


TIMU ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina nyota wake wanne wameitwa kuunda kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Kocha Mkuu wa Stars, Kim Poulsen amesema kuwa ametazama nguvu ya wachezaji pamoja na rekodi zao jambo ambalo limepa nafasi ya kuweza kuwachagua wachezaji hao.

Pia ameongeza kuwa amezungumza na makocha kuhusu maendeleo ya wachezaji hao na imani yake ni kuonakwamba watapata matokeo chanya.


Stars inatarajiwa kuingia kambini Machi 8 ambapo itakaa kwa muda wa kati ya siku tano ama sita kabla ya kuelekea Kenya kucheza mechi za kirafiki.

Malengo ya kambi hiyo ni maandalizi ya mechi za kufuzu Afcon, nyota hao ni hawa hapa:-Laurent Alfred (Azam FC, Under 20), Ayoub Lyanga, Salum Aboubakar ‘Sure boy’, Iddi Seleman ‘Nado’ (Azam FC).


ORODHA YA NYOTA NANE WA YANGA NDANI YA TAIFA STARS SAMATTA Sr :- HUYU MIQUISSONE HUYUU..!!

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply