Yanga SC

WAZIR JUNIOR AJIPA MATUMAINI YA KUFANYA VIZURI YANGA

admin February 28, 2021 12:47 pm


 WAZIR Junior mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa anachopitia kwa sasa ni suala la muda ana amini kwamba atapata nafasi ya kucheza.

Kwenye usajili wa dirisha dogo, timu zaidi ya tano ikiwa ni pamoja na KMC, Coastal Union, Gwambina na Namungo zilikuwa zinahitaji huduma yake kwa mkopo ia dili lake libuma baada ya Kocha Mkuu,Cedric Kaze kuhitaji huduma yake.

Junior ambaye ni ingizo jipya kutoka Klabu ya Mbao FC bado hajawa na nafasi kikosi cha kwanza zaidi ya kujenga ushkaji na benchi.

Nyota huyo amesema:”Ilikuwa niondoke wakati ule wa dirisha dogo ila mwalimu alitaka nibaki hivyo nina amini kwamba bado nina nafasi ya kufanya vizuri.

“Kikubwa ni kuendelea kupambana ili kuwa bora kwa kuwa ushindani ni mkubwa na kila kitu nina amini kwamba kila kitu kitakuwa sawa,”.

Ndani ya Yanga ametupia bao moja ilikuwa mbele ya KMC wakati Yanga ikishinda 2-1.

BEKI SIMBA ABADILISHIWA MAJUKUMU BARBARA: UWEKEZAJI WA KWELI UNALETA MAFANIKIO KWENYE SOKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply