Home Simba SC AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA...

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO


RAHEEM Kangezi,’Zamuda’ Mwenyekiti wa Klabu ya African Lyon na mmiliki wa timu hiyo amesema kuwa wamefanya mambo mengi kwa ajili ya Simba ikiwa ni pamoja na logo mpya ya timu hiyo pamoja na mpango wa Visit Tanzania.

Zamuda amesema kuwa ikiwa wanasema kwamba anapiga porojo hilo sio kweli kwa kuwa anamheshimu kila mtu ikiwa ni pamoja Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.

Jana timu yake ilipoteza kwa kufungwa 0-3 dhidi ya Simba huku akiweka wazi kwamba kuna vitu aliahidiwa kulipwa na bosi wa timu yao ila havijafanyika mpaka sasa. 

“Tunafanya vitu vingi sana ndani ya Simba kwa kuwa ile Visit Tanzania imetoka kwetu na muulize Barbra (Gonzalez) akuonyeshe email ambayo nilimtumia pia logo mpya ya Simba imetoka kwetu.

“Tuna wachezaji ndani ya ligi zaidi ya 50, Miraji Athuman ametoka kwetu, kuna Mwenyekiti wa Mashindano wa Yanga ametoka kwetu na kocha msaidizi pia ametoka kwetu.

“Bajeti yetu sio kubwa lakini ni tofauti kidogo kwa kuwa ninawalipa wachezaji na ninasafirisha wachezaji na kusomesha pia,” amesema.

SOMA NA HII  OKRAH AFUNGUKA KILICHOMVUTA YANGA....AMTAJA 'MBAYA WA SIMBA'....