Home news BREAKING:MECHI ZOTE ZA NAMUNGO DHIDI YA WAANGOLA KUPIGWA BONGO

BREAKING:MECHI ZOTE ZA NAMUNGO DHIDI YA WAANGOLA KUPIGWA BONGO

 


SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeamua mechi zote mbili za Kombe la Shirikisho kati ya CD 1 Agosto ya Angola na Namungo FC ya Tanzania zichezwe nchini Tanzania.


Uamuzi huo umefanywa baada ya Kamati ya CAF ya Mashindano hayo kubaini kuwa si Agosto wala Namungo iliyohusika moja kwa moja kukwamisha mechi ya kwanza iliyokuwa ichezwe Februari 14 nchini Angola.

Mechi zote mbili zinatakiwa kuchezwa angalau ndani ya saa 72, na ziwe zimechezwa kufikia Februari 26 mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba, CD 1 Agosto itakuwa mwenyeji wa mechi ya kwanza, hivyo itawajibika katika maandalizi yote ikiwemo gharama za maofisa wa mechi hiyo.

Kwa vile makundi ya Kombe la Shirikisho yatapangwa Februari 22, mshindi wa jumla baada ya mechi hizo mbili hatazingatiwa katika viwango (non-ranked) wakati wa upangaji.


Mechi hiyo iliahirishwa kwa kile ambacho kilielezwa kuwa mamlaka ya Angola iliwataka wachezaji wote wawekwe karantini baada ya wachezaji watatu pamoja na kiongozi mmoja wa Namungo kuelezwa kuwa wamekutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona.

    Baada ya Namungo kugomea jambo hilo mamlaka ya Soka ya Tanzania, (TFF) walifuatilia kwa pamoja ili kupata ukweli wa mambo mpaka pale Caf ilipoamua kufuta mchezo huo wa kwanza ugenini.

Hivyo kwa taarifa iliyotolewa na TFF leo Februari 17 ni rasmi Namungo atakuwa nyumbani kwenye mechi zote mbili ndani ya Bongo. 
SOMA NA HII  SIMBA YATAJA SIRI ...MWARABU ANAKUFA DAR..MORRISON KUPANGUA KIKAOSI...MHILU AFUNGUKA MAPYA ...