Home kimataifa WAAFRIKA WAWILI WAKIWASHA LIGI YA MABINGWA ULAYA

WAAFRIKA WAWILI WAKIWASHA LIGI YA MABINGWA ULAYA


 RAIA wawili wa Afrika wanaocheza ndani ya England, Mohamed Salah na Sadio Mane waliweza kutimiza majukumu yao ya kutupia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa jana, Puskas Arena.

Wakiwa chini ya Kocha Mkuu, Jurgen Klopp, Mohamed Salah, raia wa Misri na Saidio Mane raia wa Senegal walipeleka maumivu kwa Klabu ya RB Leipzig kwa ushindi wa mabao 2-0.

Ndani ya dakika tano waliweza kufunga mabao hayo mawili ambapo Salah alianza kufunga bao la kwanza dakika ya 53 kisha Mane akatupia bao la pili dakika ya 58.

Ushindi huo unaifanya Liverpool ambayo beki yao inapata shida kutokana na wachezaji wake wengi kusumbuliwa na majeraha inakuwa na matumaini ya kusonga mbele ndani ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa watafanikiwa kulinda ushindi huo kwa namna yoyote wakiwa nyumbani, Anfield.

Klopp amesema kuwa ni mwanzo mzuri kwa vijana wake na wamepambana kufikia ushindi huo wakiwa ugenini.

SOMA NA HII  JOSE MOURINHO SASA NI MALI YA AS ROMA