Home Yanga SC CARLINHOS AKABIDHIWA MAJUKUMU YA SAIDO YANGA

CARLINHOS AKABIDHIWA MAJUKUMU YA SAIDO YANGA

 

KOCHA mkuu wa Yanga, Cedrick Kaze amesema kuwa kurejea kwa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Carlos Carlinhos kutaongeza ubora katika kikosi chake ambacho kinaendelea kumkosa nyota Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’.

Yanga jana Jumamosi ilikuwa na kibarua kizito katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo walimenyana dhidi ya Mbeya City, mchezo ulioisha kwqa sare ya bao 1-1. 

Katika mchezo wa mzunguko kwanza kwa timu hizo, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 liliofungwa na beki Lamine Moro huku pasi ya bao ikitolewa na kiungo Carlos Carlinhos.

Akizungumzia kurejea kwa nyota huyo raia wa Angola Kaze alisema kukosekana kwa Saido katika kikosi cha Yanga ni habari mbaya lakini anaamini uwepo wa Carlinhos utaisaidia timu hiyo  kufanya vizuri.

“Saido atakosekana kutokana na kutokuwa fiti,hii si habari njema kwa wanayanga wote kwa kuwa wanafahamu uwezo wa Saido, lakini naamini bado kuna wachezaji wazuri ndani ya Yanga ambao wanaweza kucheza na kuisadia timu kufanya vizuri.

“Nafurahi kuona Carlos Carlinhos amerejea katika kikosi, ni mchezaji mzuri ambaye pia hucheza katika nafasi ambayo hucheza Saido na akafanya vizuri, tunatarajia kupata ubora na huduma nzuri kutoka kwake kama ilivyo kwa wachezaji wengine wa Yanga,”

SOMA NA HII  MWAMBA HUYU HAPA ALIYECHUKUA MIKOBA YA MAYELE