Home Simba SC GOMES AWAKAZIA MAZEMBE, ATAJA SABABU ZA SARE NA KUSEPA NA KOMBE

GOMES AWAKAZIA MAZEMBE, ATAJA SABABU ZA SARE NA KUSEPA NA KOMBE


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapinzani wao TP Mazembe walikuwa imara muda wote jambo ambalo limewafanya waambulie sare kwenye mchezo wao wa mwisho kwenye mchezo wa Simba Super Cup.

Licha ya Gomes kuwakazia wababe hao kwenye soka la Afrika, TP Mazembe bado timu yake iliweza kuibuka vinara kwenye mashindano ya Simba Super Cup kwa kukusanya pointi nne huku TP Mazembe wakiwa nafasi ya tatu na pointi yao ni moja.

Kwenye mashindano hayo ambayo ni mara ya kwanza kufanyika kwenye bara la Afrika, Simba walianza kufungua kwa ushindi wa mabao 4-1 Januari 27 dhidi ya Al Hilal ambao wao ni washindi wa pili baada ya kuifunga mabao 2-1 TP Mazembe. 

Mchezo wa jana,Januari 31 Simba ikiwa Uwanja wa Mkapa, ulikamilika kwa sare ya bila kufungana huku Simba ikikosa nafasi nyingi za wazi kupitia kwa kiungo wao Clatous Chama aliyekosa nafasi nne huku mshambuliaji Chris Mugalu akikosa nafasi mbili.

Kuhusu sare hiyo Gomes amesema:”Haikuwa bahati yetu kwani tulikutana na upinzani mkubwa kutoka kwa TP Mazembe, jambo zuri ni kwamba hatujafungwa ni mwanzo wa kujifunza pia.

“Wachezaji wanafanya vizuri wanastahili pongezi nina amini kwamba tutakuwa vema katika mechi zetu zijazo, shukrani kwa mashabiki kwa sapoti yao,” .

Mashindano hayo yalikuwa maalumu kwa ajili ya kikosi cha Simba kujiaandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo imetinga hatua ya makundi.

Pia timu zote mbili shiriki ambazo ni Al Hilal na TP Mazembe zimetinga hatua ya makundi ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  SIMBA YATUMA UJUMBE KWA POLISI TANZANIA