Home Simba SC SIMBA YATUMA UJUMBE KWA POLISI TANZANIA

SIMBA YATUMA UJUMBE KWA POLISI TANZANIA


UONGOZI wa Simba umeweka wazi kwamba upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi Polisi Tanzania unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi, Juni19.

Tayari kikosi cha Simba kipo Moshi ambapo kiliwasili jana, Juni 16 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 2-0 Polisi Tanzania hivyo kisasi kwa Polisi itakuwa kushinda na Simba itakuwa na kazi ya kulinda rekodi zake.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi hiyo pamoja na zote ambazo zimebaki.

“Tupo tayari kwa ajili ya mechi zetu na kila mmoja anajua kwamba tunahitaji pointi tatu. Kikubwa ni kuona kwamba tunashinda kwani hilo ni jambo muhimu.

“Mashabiki watupe sapoti kwa ajili ya mchezo huo na tunatambua kwamba utakuwa ni mgumu kwa kuwa tunakutana na timu nzuri,” amesema.

Kwenye msimamo wa ligi, Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 67 baada ya kucheza 27, inakutana na Polisi Tanzania iliyo nafasi ya 7 na pointi 41. 

SOMA NA HII  ZA NDAAANIII KABISA....BARBARA , MKWABI KUCHUKUA NAFASI YA TRY AGAIN SIMBA...