Home Simba SC UHAKIKA: SIMBA YASHUSHA MBADALA WA MKUDE KUTOKA MALI..

UHAKIKA: SIMBA YASHUSHA MBADALA WA MKUDE KUTOKA MALI..


SIMBA wanatafuta kiungo wa juu ‘namba nane’ mwenye uwezo mkubwa wa kukaba na kushambulia ili aje kucheza sambamba na Taddeo Lwanga ambaye ni kiungo mkabaji.

Simba tayari mezani wana majina ya viungo watatu lakini hakuna hata mmoja aliyepita moja kwa moja kutokana na sababu mbalimbali.

Viungo hao ni Zubery Dabi na Shaban Msala wote wanacheza Ruvu Shooting pamoja na kiungo mwingine anayetumia mguu wa kushoto Mmali na anacheza timu ya taifa ya nchi hiyo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa Didier Gomes alitoa pendekezo la Mmali Sadio Kanoute akasajiliwa na Al-Ahli Benghazi ya Libya, baada ya kumkosa akampendekeza kiungo mwingine kutoka katika nchi hiyo ambaye anacheza timu ya taifa na anatumia mguu wa kushoto.

“Wazawa Dabi na Msala wote suala lao la kuwasajili limekuwa gumu,kulingana na mahitaji shida ya kwanza kwetu ni kiungo namba nane anayeweza kukaba na kushambulia.

“Nasi tutapendekeza wawili wengine na watakuwa watatu kisha tutakaa chini kwa pamoja na Gomes, kuwapambanisha yule ambaye atakuwa bora zaidi ya wote kulingana na mahitaji ya timu ndio tutamsajili,”alisema kiongozi mmoja wa kamati ya usajili ya Simba.

Katika hatua nyingine, kikosi cha Simba cha Simba kimewasili salama mkoani Mwanza kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania ambayo itachezwa Jumamosi ijayo, katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

SOMA NA HII  SIMBA KUKIPIGA MECHI YA KIRAFIKI NA WALIOWAHI KUWAFUNGA GOLI 5....NGOMA ITACHEZWA CAIRO KWENYEWE KULEEE...