Home news KUELEKEA MECHI YA KESHO…KUMBE PABLO ALISHAWAMALIZA WAARABU KITAMBO SANAAH…KISINDA AMJIBU…

KUELEKEA MECHI YA KESHO…KUMBE PABLO ALISHAWAMALIZA WAARABU KITAMBO SANAAH…KISINDA AMJIBU…


KATIKA kuhakikisha analipa kisasi cha mabao 2-0 ilichopewa Simba ugenini na RS Berkane, Kocha wa Simba, Pablo Franco ametumia muda mfupi uliosalia kuwachora wapinzani wao hao kutoka Morocco.

Pablo ametumia muda wake na wasaidizi wake kuwasoma Berkane kupitia video za mechi zao ukiwamo ule wa baina yao uliopigwa Morocco, ili kupata dawa ya kuwamaliza Kwa Mkapa.

“Miongoni mwa vitu tulivyoona wanapokuwa nyumbani wapo tofauti na ugenini, huwa wanazuia zaidi na kumiliki mpira zaidi ili kujilinda na hata kushambulia kwao ni kwa nidhamu si kama inavyokuwa nyumbani,” alisema.

“Kuna mengi ya kiufundi zaidi tumeona kutoka kwao katika kuwafuatilia si vyema kuweka wazi ila tunayafanyia kazi yote na naimani tutacheza kwa mabadiliko makubwa na tutapata matokeo mazuri dhidi yao,” aliongeza Pablo.

Aidha winga wa RS Berkane, Tuisila Kisinda alisema wanafahamu mechi ya Jumapili, itakuwa ngumu pengine zaidi ya kule kwao ila wanachohitaji kupata ni pointi.

SOMA NA HII  ISHIKILIE SLOT YA THIRSTY VIKING KWENYE MERIDIANBET CASINO KWA UHAKIKA WA MAOKOTO...