Home Habari za michezo KISA YANGA KUWA NA POINT 13 CAF….JEMEDARI ‘MCHAMBA’ MANARA KWA HILI…AMUITA MPUUZI…

KISA YANGA KUWA NA POINT 13 CAF….JEMEDARI ‘MCHAMBA’ MANARA KWA HILI…AMUITA MPUUZI…

Habari za Yanga

Mchambuzi wa soka nchini, Jemedari Said Kazumari amesema kuwa kitendo cha Msemaji wa Yanga, Haji Manara kudai kuwa yanga ndiyo timu pekee Tanzania kuwahi kuongoza Makundi na Kufikisha alama 13 mashindano ya CAF ni upotoshaji.

Manara alitoa kauli hiyo kufuatia ushindi wa Yanga dhidi ya TP Mazembe katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na kuongoza kundi D jambo ambalo si kweli kwani msimu wa 2020/2021 watani wao wa jadi Simba katika michuano ya Mabingwa Afrika waliongoza kundi mbele ya Al Ahly na kupata alama hizo 13.

“Simba ilifikisha alama kumi na tatu (13) kwenye mashindano ya vilabu magumu kupita yote barani Afrika.

“Ukisikia mpuuzi yoyote anakuambia alama 13 za Yanga kwenye kombe aliloliita la “luza” kuwa ni rekodi ya Taifa na hakuna klabu yoyote Tanzania imewahi kufanya hivyo kwa mashinadno ya vilabu Afrika.

“Mkalie mbali na mpuuze tu kwakuwa inawezekana ni kweli kuna wenye akili 2 tu huko aliko Kama alivyowahi kusema yeye mwenyewe.

“Hawa ndo wanaitaga press wakasema eti wanawazidi Waandishi kwakuwa wao wanafanya tafiti, pumbaavu kabisa,” amesema Jemedari Said Kazumari.

SOMA NA HII  KISA SAFARI YA ZANZIBAR ALLY KAMWE AMPIGA KIJEMBE FEI TOTO