Home Habari za michezo KUELEKEA DARBI….MAYELE KAMTAZAMA ONYANGO WEE….KISHA AKATIKISA KICHWA NA KUSEMA HAYA…

KUELEKEA DARBI….MAYELE KAMTAZAMA ONYANGO WEE….KISHA AKATIKISA KICHWA NA KUSEMA HAYA…

Habari za Simba

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amewachimba mkwara mabeki wa Simba akiwemo Josh Onyango kwa kuwaambia moja ya kazi kubwa iliyopo mbele yake kwa sasa ni kuhakikisha anapata nafasi ya kuifunga timu hiyo katika Ligi Kuu Bara kuelekea mchezo wao wa Aprili 16, mwaka huu.

Mayele ametoa kauli hiyo kufuatia rekodi yake katika Ligi Kuu Bara kushindwa kuifunga timu hiyo kwenye mechi za ligi kuu licha ya kuwafunga mara mbili katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

Yanga ambao wanaongoza ligi wakiwa na pointi 65 wakifuatiwa na Simba wanaokamata nafasi ya pili wenye pointi 57, watakutana Aprili 16, mwaka huu katika mchezo ligi ambao unatarajiwa kupigwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza nasi, Mayele alisema kuwa anajua ubora wa safu ya ulinzi wa Simba lakini moja ya malengo yake msimu huu ni kuhakikisha anafanikiwa kuwafunga katika mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara msimu ili kuweza kufikia malengo yake.

“Najua haitokuwa mechi rahisi kwa sababu wao wanatujua vizuri kama sisi tunavyowajua wao na ukiangalia hii ni mchezo ambao unaenda kukutanisha watani, presha inakuwa kubwa kwa sababu kila upande unahitaji kuona unapata matokeo mazuri ili kulinda heshima ya klabu katika mchezo wa aina hii.

“Binafsi nimeshazoea kucheza dhidi yao lakini tayari nimeshawafunga mara mbili katika mechi za Ngao ya Jamii ingawa bado kuna kitu sijakitimiza hasa upande wa ligi kuu dhidi yao, nataka kuona nafanikiwa kuweza kufunga katika mchezo wetu ujao japo kuwa haitokuwa kitu rahisi kutoka na mabeki imara waliokuwa nao,” alisema Mayele.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA TP MAZEMBE...THOMAS ULIMWENGU AILENGESHEA YANGA...AANIKA SIRI ZA WACONGO...