Home Uncategorized SIMBA YATOA TAMKO RASMI KUHUSU DABI KUSONGEZWA MBELE

SIMBA YATOA TAMKO RASMI KUHUSU DABI KUSONGEZWA MBELE

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa hauna mamlaka ya kuzungumzia kuhusu kupelekwa mbele mchezo wao wa Ligi Kuu Bara kati yao na Yanga uliotarajiwa awali kuchezwa Oktoba 18.


Leo, Oktoba 7 taarifa rasmi kutoka Bodi ya Ligi Tanzania,(TPLB) imeeleza kuwa mechi hiyo itachezwa Novemba 7 sababu kubwa ikiwa ni uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa vikwazo katika usafiri wa kimataifa baada ya kukamilika kwa michezo ya kimataifa iliyopo kwenye kalenda ya FIFA jambo ambalo linaweza kuathiri wachezaji wa vikosi wa timu hizo mbili.

Mchezo huo umepelekwa mbele mpaka Novemba,7 2020, Uwanja wa Mkapa na utachezwa saa 11:00 jioni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema:-“Simba muda wote tunaamini katika maamuzi ya wenye mamlaka ya mpira siku zote.

“Kila mtu anataka kujua juu ya neno kutoka Simba, sisi tuna msimamo wetu na imani yetu, Klabu ya Simba inaamini katika kile kinachopangwa na wenye mpira.

“Tumekubaliana na tumekubali katika maamuzi yanayofanywa na vyombo, Bodi ya Ligi, Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) sisi muda wote tunaamini katika kile ambacho kinapangwa.

“Yale yanayopangwa na Bodi ya Ligi, Simba haina uwezo wa kupinga mamlaka, wenye mpira wao ni TFF na Bodi ya ligi wao wakiamua sisi hatuna cha kufanya.


“Kazi yetu sisi Simba ni kucheza mpira, hatuhusiki na masuala ya kupanga ratiba hiyo haituhusu sisi, tutafanya kile ambacho tunaambiwa, hatuna kauli na hatuwezi kubadilisha ratiba.” 


SOMA NA HII  NAMUNGO HESABU ZAO NDANI YA LIGI KUU BARA