Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA TP MAZEMBE…THOMAS ULIMWENGU AILENGESHEA YANGA…AANIKA SIRI ZA WACONGO…

KUELEKEA MECHI NA TP MAZEMBE…THOMAS ULIMWENGU AILENGESHEA YANGA…AANIKA SIRI ZA WACONGO…

Habari za Yanga

Aliyekuwa mshambuliaji wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu, amesema Yanga inaweza kutoka na ushindi kwenye mchezo wao ujao wa makundi dhidi ya Tp Mazembe kama ikiutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani.

Yanga imeanza vibaya kwenye mchezo wake wa kwanza katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa 2-0 na Us Monastir nchini Tunisia.

Akizungumza Ulimwengu ambaye timu yake ya mwisho kuitumikia ilikuwa Mazembe alisema Yanga wakitulia wana uwezo wa kutoka na ushindi katika mchezo wao wa nyumbani dhidi ya TP Mazembe utakaochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Februari 19.

“Mechi itakuwa nzuri na ngumu ila Yanga ina nafasi ya kushinda kama itatumia uwanja wa nyumbani vizuri, kila kocha ana mfumo wake wa maandalizi kwenye mechi hizi.

“Najua makocha wengi kabla ya mechi huwa wanaangalia wapinzani wao kwa hiyo najua upande wa Yanga, nahisi atakuwa kashaangalia na atakuwa anajua yupi hatari zaidi kwa Mazembe.”

Ulimwengu ambaye kwa sasa yupo hapa jijini Dar es Salaam, aliongeza; “Yanga ina wachezaji wazuri na Mazembe pia ina wachezaji wazuri kwa hiyo nahisi mchezo utakuwa mzuri sana.

Ulimwengu ni miongoni mwa wachezaji waliochukua Kombe la Ligi ya Mabingwa akiwa na TP Mazembe.

Mshambuliaji huyo aliachana na Mazembe msimu uliopita baada ya kumaliza mkataba wa kuitumikia timu hiyo na sasa anafanya mazoezi binafsi jijini Dar.

SOMA NA HII  BEKI WYDAD CASABLANCA AWAOGOPA SIMBA...AVUNJA UKIMYA...ISHU NZIMA IKO HIVI