Home Habari za michezo MSUVA AWAPA SIMBA AKILI YA KUCHEZA NA WAARABU…AFUNGUKA MAENEO YA KUKAMIA…

MSUVA AWAPA SIMBA AKILI YA KUCHEZA NA WAARABU…AFUNGUKA MAENEO YA KUKAMIA…

Saimon Msuva

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ambaye aliwahi kucheza soka la kulipwa Morocco akiwa na Wydad Casablanca, amewataka Simba kuandaa mpango wa kumdhibiti winga hatari wa Raja Casablanca, Zakaria Habti, kwenye mchezo wao ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa Jumamosi ijayo.

Lakini jingine;”Jambo muhimu kwa Simba ni kucheza kwa tahadhari, huku wakiishambulia bila ya kuwapa nafasi maana wakitangulia kupata wao bao mchezo unaweza kuwa mgumu, jamaa wanajua kupoteza muda sana na hilo Simba wanatakiwa kuwa nalo makini sana.”

Wapinzani hao wa Simba kwenye kundi C, walikuwa wapinzani wa Msuva wakati akicheza soka la kulipwa nchini humo akiwa na kikosi cha Difaa Jadida na baadaye kwenda Wydad kabla ya kuingia kwenye mvutano na kimaslahi na klabu hiyo na kuamua kuachana nayo huku akitimkia Saudi Arabia.

Licha ya kwamba Raja Casablanca ina sura chache mpya kutokana na kuondoka kwa Ben Malango na Soufiane Rahimi, Msuva alisema bado staili yao ya uchezaji ni ileile.

“Wapo wachezaji ambao nilishindana nao mfano ni huyo, Zakaria ni hatari sana, siyo mchezaji wa kumwachia nafasi, nimesikia kuwa bado anaendelea kufanya vizuri nafikiri Simba wanatakiwa kuhakikisha wanamuundia mkakati maalumu vinginevyo atawapa madhara,”

“Wakati nikiwa Morocco, walikuwa na mshambuliaji wao mmoja hivi, anaitwa Malango huyo jamaa alikuwa analijua sana goli, nakumbuka msimu wangu wa mwisho kule, nilifunga mabao saba, yeye alifunga mabao 16, kwa sasa yupo Qatar kitu kama hicho,”

mchezaji huyo wa zamani wa Yanga, aliongeza kwa kusema, mbali na Zakaria mchezaji wao mwingine ambao ameona wanafanya vizuri ni pamoja na Abdelilah Hafidi, Yousri Bouzok, Mohammed Nahiri na Hamza Khabba.

“Jambo muhimu kwa Simba ni kucheza kwa tahadhari, huku wakiishambulia bila ya kuwapa nafasi maana wakitangulia kupata wao bao mchezo unaweza kuwa mgumu, jamaa wanajua kupoteza muda sana na hilo Simba wanatakiwa kuwa nalo makini sana.”

Wakati akiwa na Wydad Casablanca, Msuva ambaye ni mchezaji tegemeo wa timu ya Taifa, Taifa Stars alikutana na Raja Casablanca mara mbili kwenye michezo ya Ligi Kuu Morocco ambayo ni maarufu kama Batola Pro na hakuwahi kufunga bao dhidi yao, lakini akiwa na Difaa El Jadida timu yake ya kwanza kuichezea nchini humo, aliwafunga na kutoa asisti mara moja.

Raja Casablanca ambao kwenye mchezo wao wa kwanza wa makundi walitoa dozi kwa mabingwa wa Uganda, Vipers ya mabao 5-0, wana mchezaji wa Kitanzania, Adrian Kitare lakini yupo kwenye timu zao za vijana.

SOMA NA HII  USAJILI WA KWANZA YANGA HUU HAPA...BOSI AMPANDIA NDEGE..PABLO AKUBALI MZIKI WAO...