Home Habari za michezo BAADA YA MAISHA YA SIMBA KUWA MAGUMU….MKUDE HUYOOO SINGIDA BIG STARS….DILI ZIMA...

BAADA YA MAISHA YA SIMBA KUWA MAGUMU….MKUDE HUYOOO SINGIDA BIG STARS….DILI ZIMA LIKO HIVI…

Habari za Simba leo

Klabu ya Singida big stars imetuma maombi ya kuhitaji huduma ya kiungo mkabaji wa Simba SC Jonas Mkude.

Usajili huo utakamilika mwishoni mwa msimu kama makubaliano yatafikiwa baina ya pande hizo mbili.

Vilevile Ihefu FC imeonyesha nia ya kuvutiwa na Kiungo huyo ambae inaonekana kupata namba ndani ya Simba imekuwa changamoto.

Toka kuanza kwa msimu huu, Mkude amekuwa hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza  cha Simba, huku Mzamiru Yasin akionekana kuimarika siku hadi siku.

Mkude ni mchezaji pekee aliyebaki klabuni hapo kwa zaidi ya misimu 10 ya soka, ambapo kwa mara ya kwanza yeye pamoja na wenzake Ibrahim Ajib na Said Ndemla walipata nafasi ya kucheza msimu wa 2009/2010.

Hata hivyo Mkude amekuwa na kiwango cha shuka panda kwa misimu yote hiyo, huku mara kadhaa akikoswa koswa kuachwa kwenye madirisha ya misimu ya nyuma.

Tayari, wakongwe wenzake (Ajib na Ndemla) kwa nyakati tofauti walishatafuta maisha mapya nnje ya Simba, ambapo wote wawili hivi sasa wanacheza Singida Big Stars .

SOMA NA HII  RAIS KENYATTA ATOA ZAWADI YA MILIONI MIANNE KWA 'SIMBA NA YANGA' ZA KENYA....