Home Habari za michezo YANGA SC WAAMBIWA WAKAMCHUKUE FEI TOTO ZANZIBAR…ISHU IKO HIVI…

YANGA SC WAAMBIWA WAKAMCHUKUE FEI TOTO ZANZIBAR…ISHU IKO HIVI…

Tetesi za Usajili Yanga

KOCHA wa KVZ, Amri Said amesema kama zipo timu za Ligi Kuu Bara zina uhitaji wa viungo na washambuliaji wenye vipaji vikubwa basi amezishauri zifike Zanzibar ambako vimejaa tele.

Tangu atue Zanzibar kukinoa kikosi hicho, alisema ameviona vipaji vikubwa ambavyo kama kuna timu ya Bara inahitaji itume maskauti wa kuvifuatilia na anaamini itafaidika hata kwa kuviuza kwa bei ya juu.

“Viungo kama kina Feisal Salum ‘Fei Toto’ vipo kibao shida timu nyingi hazina uvumilivu wa kuvifuatilia vikianza kujulikana ndio wanaanza kung’ang’aniana, jambo ambalo halisaidii mpira wetu.

“Kama watatokea viongozi watakaoamua kujenga timu yao kwa muda mrefu na yenye ushindani, nawashauri wawe na watalamu watakaotenga muda wao kwa ajili ya kufuatilia vipaji sehemu mbalimbali.”

Alisema kinachotakiwa kwa vipaji vilivyopo Zanzibar hasa viungo na washambuliaji aliowataja ni motisha kutokana na wachezaji hao kucheza kwa kujifurahisha kutokana na maslahi madogo wanayoyapata.

“Kiukweli Ligi Kuu Bara ina sapoti kubwa sana, ndio maana wachezaji wengi wanapata morali ya kucheza kwa bidii, tofauti na huku licha ya vipaji vikubwa ila naona kama maslahi yake yapo chini, jambo ambalo linawafanya wacheze kwa mapenzi na siyo kazi,” alisema.

Amri ambaye timu yake ni kinara wa ligi hiyo ya Zanzibar alisema yapo mambo aliyojifunza baada ya kufundisha Bara na Visiwani anayotamani kuyafanyia kazi ili kutoa mchango wake kuhakikisha soka linasonga mbele.

“Moja ya vitu vikubwa nilivyojifunza ni kufuatilia na kuwa na misingi ya kuwajenga wachezaji kwa sababu soka kwa nyakati hizi lina pesa kwa wachezaji ambao watajituma na kuliona hilo,” alisema.

Hivi karibuni, Kiungo Fei Toto alivunja mkataba wa kuitumikia Yanga SC kwa kile kilichodaiwa kuwa anataka kupata changamoto mpya ya kisoka.

Hata hivyo, duru za micehzo nchini zinahusisha tukio hilo na klabu ya Azam FC ambao inasemekana wanampango wa kumsajili kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.

Fei Toto alilazimika kulipa kiasi cha Tsh Milioni 112 ili kuvunja mkataba wake na Yanga SC kama sehemu ya mkataba huo unavyobainisha ikiwa mchezaji angetaka kuvunja mkataba wake.

SOMA NA HII  WALICHOFANYA INONGA NA MAYELE KWA MASHABIKI WA YANGA JUZI...KILA MMOJA ALIWAINUA KUSHANGILIA..