Home Simba SC HAJI MANARA: STRESS NADHANI ZIPO KWA YANGA,UCHAGUZI KUFANYIKA KESHO

HAJI MANARA: STRESS NADHANI ZIPO KWA YANGA,UCHAGUZI KUFANYIKA KESHO


 OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa anaamini watani zao wa jadi Yanga, wana stress, (presha) kutokana na kuona timu hiyo ikifanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na kuingia mikataba mbalimbali.

Kumekuwa na majibizano kwenye mitandao ya kijamii kati ya Ofisa Habari wa Simba, Manara kuhusu namna hali yake ya utani ilivyo kwa mashabiki wa Yanga ambapo alipandisha picha kwenye mtandao wa kijamii ukiwa na jezi ya Yanga pamoja na Simba.

Baada ya Manara kupandisha jezi hizo mashabiki ambao inaaminika ni wa Yanga walitoa maoni yao wakimponda Manara kutokana na jambo hilo huku wakiamini kwamba ni utani uliopitiliza.

Kupitia kwenye mkutano na waandishi wa habari leo Februari 6, Manara amesema:-“Msemaji wao aliwahi kusema kuwa jezi ya Simba ni takataka, hazifai hatakufutiwa viatu je mliskia Simba tukilalamika?

 “Hatujawahi Simba kulalamika, pia hivi karibuni jezi ya Simba iliweza kuchomwa moto.Watu walishangilia lakini hakuna aliyesimama kuzungumzia hili pia.

“Sasa vipi hawa Yanga wanakuaje, wanalalamika kwa nini?Simba mliwahi kuskia wanalalamika. Sasa vipi Yanga ninachokiamini ni stress za matokeo, stress za kuona Simba Super Cup imefanikiwa, stress za kuona Simba inatwaa ubingwa mara ya nne.

“Stress za kuona Simba inatinga hatua ya robo fainali ndio katika hili hakuna matatizo inafanikiwa, stress za kuona Simba inaingia mikataba kila kukicha,” .

Pia Manara amesema kuwa anaamini kuwa wanachama wa Klabu ya Simba kesho watafanya maamuzi sahihi kwenye uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti iliyoachwa wazi na Sued Mkwabi aliyebwaga manyanga.

Wagombe ambao wanawania nafasi hiyo ni Juma Nkamia na Murtaza Mangungu.


SOMA NA HII  HII HAPA TAARIFA MPYA KUHUSU VYUMA VINGINE VITAKAVYOSHUKA SIMBA....