Home Yanga SC KAZE ARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA YANGA DHIDI YA MBEYA CITY

KAZE ARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA YANGA DHIDI YA MBEYA CITY

 


KOCHA mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amefunguka kuwa ameridhishwa na maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wao dhidi ya Mbeya City utakaopigwa siku ya Jumamosi.

Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa ligi na pointi zao 44 walizokusanya katika michezo 18 waliyocheza mpaka sasa wakishinda mechi 13 na kutoa sare kwenye michezo mitano.

Kuelekea mchezo huo Yanga imecheza michezo miwili ya kujipima nguvu ambapo imeshinda mchezo mmoja dhidi ya timu yao ya vijana U20, na kupoteza mchezo mmoja mbele ya African Sports.

Akizungumzia maandalizi hayo, Meneja wa kikosi cha Yanga, Hafidh Saleh amesema baada ya kucheza michezo miwili ya kirafiki, kocha wa klabu hiyo Cedric Kaze ameridhishwa na maendeleo ya nyota wake.

“Kikosi kinaendelea vizuri na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Mbeya City utakaopigwa siku ya Jumamosi, kocha Kaze anaonekana kuridhishwa na viwango vya nyota wake baada ya wiki mbili za mazoezi tangu tulivyoanza rasmi kambi Januari 25.

“Tunajua mchezo dhidi ya Mbeya City utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunafanikiwa kupata ushindi katika mchezo huo, tumepata michezo ya kirafiki ambayo imempa kocha mwanga wa wapi tumeimarika na wapi bado tunaonekana kuwa na mapungufu,”

SOMA NA HII  ZA NDAANI KABISA YANII....MRITHI WA SENZO YANGA HUYU HAPA....KAFANYA MAKUBWA SANA DR CONGO...AKITUA ANAANZA NA HILI...