KOCHA Mkuu wa Al Ahly ya Misri amesema kuwa anawatambua vema wapinzani wake Simba kwa kuwa amewafuatilia kwa muda mrefu ikiwa ni kwenye mechi zao za nyuma pamoja na ile waliyoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita,DR Congo.
Leo Uwanja wa Mkapa kutakuwa na mchezo wa kukata na shoka kati ya Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania kimataifa katika Ligi ya Mabingwa na Afrika huku kwenye upande wa Kombe la Shirikisho ni Namungo FC.
Pitso Mosimane amesema kuwa miongoni mwa wachezaji ambao anatambua ni imara ndani ya Simba ni pamoja na kiungo Clatous Chama, Luis Miquissone,Rarry Bwalya na Taddeo Lwanga.
Kocha huyo amesema:”Kuna wachezaji wazuri na tunatambua kwamba tunacheza na wachezaji wa aina gani kwa kuwa tumewafuatilia kwa muda na tunatambua namna ya kuwazuia hawawezi kutupa shida ndani ya uwanja.
“Hatuna hofu tutaingia ndani ya uwanja tukiamini kwamba kuna kitu ambacho tunakihitaji nao ni ushindi hakuna jambo jingine,”.