Home Ligi Kuu MATOKEO MABOVU YAMTISHA KOCHA MKUU WA COASTAL UNION, JUMA MGUNDA

MATOKEO MABOVU YAMTISHA KOCHA MKUU WA COASTAL UNION, JUMA MGUNDA

 


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa anatishika na mwendo ambao wanakwenda nao ndani ya Ligi Kuu Bara jambo ambalo linawafanya watulie kidogo ili kwenda sawa na kasi ya ligi.

Ikiwa ndani ya Dodoma iliyeyusha pointi sita kwa kufungwa mbele ya JKT Tanzania na Dodoma Jiji, mechi zilichezwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi zake 23 baada ya kucheza jumla ya mechi 21.

Mgunda amesema kuwa anatambua matokeo ambayo wanayapata si rafiki kwao ila watapambana kupata matokeo chanya.

“Ni kweli kwa sasa tumekuwa na matokeo ambayo si mazuri jambo ambalo linanitisha lakini kwa kuwa mimi ni mwalimu haina haja ya kuogopa haya ambayo yanatokea.

“Bado kuna mechi nyingi za kucheza na imani yangu ni kwamba tutapata matokeo chanya kwenye mechi zetu hivyo kikubwa ni wachezaji kuzidi kupambana ili kupata matokeo chanya,” amesema. 

SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI BONGO...APEWA SHAVU UBELGIJI...KUKIPIGA NA SAMATTA