Home Yanga SC YANGA KUIBUKIA MBEYA LEO, YAWAOMBA MASHABIKI WAJITOKEZE KUWAPOKEA

YANGA KUIBUKIA MBEYA LEO, YAWAOMBA MASHABIKI WAJITOKEZE KUWAPOKEA

 

KIKOSI cha Yanga leo kinatarajia kuanza safari kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City. 

Mchezo huo wa mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya ambapo Yanga wamewaomba mashabiki wao wajitokeze kwa wingi kuwapokea leo mchana Uwanja wa ndege wa Songwe, Mbeya.

Walipokutana Uwanja wa Mkapa, Yanga ilisepa na pointi tatu muhimu kwenye mzunguko wa kwanza baada ya kushinda bao 1-0 lililopachikwa na Lamine Moro. 

Februari 13 watakutana uwanjani wakiwa na mtambo wao wa mabao Fiston Abdulazack ambaye ni ingizo jipya ndani ya vinara hao wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 44.

Cedric Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na watapambana kupata matokeo chanya.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA MORRISON KUISHITAKI YANGA FIFA...UKWELI WOTE A-Z HUU HAPA....