Home Azam FC TANZANIA PRISONS YAZITAKA POINTI TATU ZA AZAM FC

TANZANIA PRISONS YAZITAKA POINTI TATU ZA AZAM FC


 UONGOZI wa Tanzania Prisons umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC utakaochezwa kesho, Februari 22, Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo ni wa mzunguko wa pili ambapo ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Azam FC ilishinda bao 1-0.

Kocha Msaidizi wa Tanzania Prisons, Shaban Kazumba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanaamini kwamba watapata pointi tatu muhimu.

“Ni mchezo wenye ushindani na mgumu ila mipango yetu ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.

“Mipango ipo sawa na kila mchezaji morali yake ni kubwa, tunahitaji ushindi ni wakati wetu wa kuona kwamba tunashinda na kupata pointi tatu muhimu,”.

Mchezo wao uliopita walipokutana mfungaji alikuwa ni Prince Dube ambaye ni kinara wa mabao ndani ya Azam FC akiwa na mabao saba.

Mchezo wao uliopita Prisons ilishinda mabao 2-1 dhidi ya KMC inakutana na Azam FC ambayo imetoka kushinda mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City.

SOMA NA HII  MAGUIRE AAMBIWA KUMKABA FULLY ZULLY MAGANGA WA RUVU NI DHARAU