Simba SC

BADO POINTI NNE SIMBA KUIFIKIA YANGA KILELENI

admin March 1, 2021 7:20 pm

SIMBA imeendelea kupunguza mlima wa kuisogelea Yanga kileleni baada ya kuichapa JKT Tanzania mabao 3-0.

Mchezo huo umepigwa leo Jumatatu ya Machi Mosi, 2021 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo Simba imefikisha pointi 45 baada kucheza mechi 19 ikiwa nyuma kwa pointi nne kwa watani wao wa jadi Yanga wenye pointi 49 baada ya kucheza mechi 21.

Simba imebakiza mechi mbili mkononi, ikishinda hizo itakuwa na pointi 51.

Kipindi cha pili, mabeki wa kati wa Simba ambao ni Pascal Wawa na Erasto Nyoni walikuwa makini kulinda zaidi langoni kwao wakisaidiana na viungo wakabaji.

Jambo ambalo liliwapa wakati mgumu washambuliaji wa JKT Tanzania,wakiongozwa na Daniel Lyanga kupiga mashuti ya kumfikia Aishi Manula.

Manula alitolewa dakika ya 71 baada ya kugongana na beki wa JKT Tanzania ambapo alipakizwa kwenye gari la kubebea wagonjwa,hivyo Beno Kakolanya aliingia kuchukua nafasi yake.

Ukiachana na mastraika hao kushindwa kupiga mashuti yakufika langoni mwao Simba, timu hiyo ilikuwa imecheza sana nyuma.

Nahodha wa Simba, John Bocco ameifungia timu yake bao la tatu dakika za nyongeza, kilichofuata ni mastaa wa Wanamsimbazi kucheza mpira wa kupaka rangi kama kuwapiga matobo na kanzu wapinzani wao.

Bocco na Kagere ngoma droo

Nahodha wa Simba, John Bocco amefikisha mabao tisa katika msimamo wa wafungaji wa Ligi Kuu Bara, baada ya leo kuifungia timu yake bao la tatu.

Mabao tisa ya Bocco ni sawa na ya straika mwenzake Mnyarwanda, Meddie Kagere.

GOMES AFUNGUKA HAYA KUHUSU MAENDELEO YA MANULA MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply