Home epl TUCHEL AWAPA TANO WACHEZAJI WAKE,UNITED WALILIA PENALTI

TUCHEL AWAPA TANO WACHEZAJI WAKE,UNITED WALILIA PENALTI


 THOMAS Tuchel, Kocha Mkuu wa Chelsea amesema kuwa pointi moja waliyopata mbele ya Manchester United,  Uwanja wa Stamford Bridge si haba kwa kuwa wachezaji walipambana kusaka ushindi.

Mchezo huo uliochezwa usiku wa kuamkia leo ulikuwa na ushindani mkubwa huku Manchester United wakilalamika kwamba walinyimwa penalti ya wazi kwenye mchezo huo uliokamika ubao kusoma 0-0.

 Mwamuzi wa kati Stuart Attwell aliikataa ambapo ilionekana nyota wa Chelsea Callum Hudson-Odoi akiugusa mpira huo walipokuwa wakipambana na Mason Greenwod na uliwagusa wote wawili kwenye mikono walipokuwa ndani ya 18.


Matokeo hayo yanaifanya Chelsea kufikisha jumla ya pointi 44 ikiwa nafasi ya 5 huku United ikibaki nafasi ya pili na pointi 50. Kinara ni Manchester City mwenye pointi 62.

SOMA NA HII  SAMUEL ETO'O KUWANIA URAIS