Simba SC

MAVITU YA DILUNGA YAMKUNA MFARANSA SIMBA

admin March 3, 2021 10:47 am


UWEZO ambao ameendelea kuuonyesha kiungo mshambuliaji wa Simba, Hassan Dilunga ndani ya kikosi hicho, umemkuna kocha wake Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa ambaye amekiri kiungo huyo amezidi kuimarika na anastahili nafasi ndani ya kikosi chake.

Dilunga alianza kwa kusuasua chini ya Gomes, lakini ameonekana kurudi kwa kasi akianza katika michezo yote miwili ambayo Simba ilicheza wiki iliyopita dhidi ya Al Ahly na African Lyon.

Nyota huyo wa zamani wa Yanga na Ruvu Shooting amefanikiwa kuhusika kwenye mabao matano ya Simba msimu huu akifunga mabao mawili na kuasisti mara tatu.

Akimzungumzia Dilunga, Gomes amesema anaridhishwa na maendeleo ya kiwango cha nyota huyo na kuahidi kumpa nafasi zaidi ya kucheza.

“Nafurahishwa sana na kiwango cha Dilunga, tangu nimekabidhiwa kikosi cha Simba mwezi uliopita, Dilunga amekuwa miongoni mwa wachezaji ambao viwango vyao vinakuwa kila siku.

“Hii ndiyo sababu mliona alipata nafasi ya kuanza  kikosi cha kwanza kwenye michezo miwili dhidi ya Al Ahly na African Lyon, na kama utaniuliza kumhusu basi nitakwambia anastahili kupata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi changu,” amesema Gomes.

NAMUNGO: TUKO TAYARI KUUWASHA MOTO SHINYANGA KAZE AOMBA KIKAO NA VIONGOZI YANGA KISA SAIDO, JOB

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply