Home Azam FC AZAM FC:HAIKUWA KAZI RAHISI KUSHINDA KAITABA, MWAMUZI ALETA UTATA

AZAM FC:HAIKUWA KAZI RAHISI KUSHINDA KAITABA, MWAMUZI ALETA UTATA


 VIVIER Bahati, kocha msaidizi wa kikosi cha Azam FC amesema kuwa haikuwa rahisi kuibuka na ushindi mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wao uliochezwa Uwanja wa Kaitaba.

Jana, Machi 3, ubao ulisoma Kagera Sugar 1-2 Azam FC na kuifanya Kagera Sugar kutimiza dakika 180 mbele ya Azam FC za msimu wa 2020/21 kwa kuwapa pointi zote sita.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Azam FC ilishinda mabao 4-2 na jana ilihitimisha mzunguko wa pili ugenini na kusepa na pointi tatu muhimu.

Mabao ya Azam FC yalifungwa na Prince Dube ambaye anafikisha bao lake la nane ndani ya ligi ilikuwa ni dakika ya 27 huku Braison Raphael yeye alifungua akaunti ya mabao ya Azam FC dakika ya 20.

Mwamuzi wa kati aliwapa mkwaju wa penalti Kagera Sugar dakika ya 42 ilijazwa kimiani na Peter Mwalyanzi huku maamuzi ya utata dakika ya 86 kwa mpira uliopigwa na Martin Kapama wa Kagera Sugar kufika kwenye mwili wa Abdul Haji,’Hamahama’ kutafsri kwamba ni faulo.

Arajiga Ahmed, alitafsri kwamba ni faulo na kuamua ichezwe nje ya 18 jambo ambalo lilionekana kuleta mkanganyiko kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Azam FC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Vivier amesema:”Haikuwa kazi nyepesi kwa vijana kuweza kupata matokeo ila mwisho wa siku wamefanikiwa.

“Akili zetu kwa sasa ni kwenye mchezo wetu dhidi ya Mwadui FC hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti kazi bado inaendelea,” .

Ikiwa imeshinda inajikita nafasi ya 3 na pointi zake ni 40 imecheza jumla ya mechi 22 huku Kagera Sugar ikiwa nafasi ya 12 na pointi zake ni 24.

Inawafuata Mwadui FC, Uwanja wa Mwadui Complex ambayo inapambana kujinasua kushuka daraja. Mwadui FC chini ya Amri Said imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Namungo.

Kwenye msimamo, Mwadui FC ipo nafasi ya 18 kibindoni ina pointi zake 15.


SOMA NA HII  KISA AZIZ KI NA CHAMA...AZAM KUZIMWAGIA MAMILIONI YA PESA SIMBA, YANGA....