Yanga SC

COASTAL UNION WAVUNJA MWIKO WA YANGA KUTOKUFUNGWA

admin March 4, 2021 3:47 pm


KLABU ya soka ya Coastal Union kutokea Tanga, leo imetamatisha mwendo wa michezo 21, bila kufungwa wa vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara klabu ya soka ya Yanga baada ya kuibuika na ushindi wa mabao 2-1.

Coastal imeibuka na ushindi huo katika mchezo mkali uliopigwa kwenye dimba la Mkwakwani jijini Tanga.

Kabla ya mchezo wa leo Yanga ilikuwa imecheza michezo 21 ya Ligi Kuu Bara, bila kupoteza mchezo wowote wakishinda michezo 14 na kutoa sare michezo saba.

 Licha ya kipigo hicho Yanga bado inasalia katika uongozi wa ligi na pointi zao 49, baada ya kucheza michezo 22.

YACOUBA AMPA JEURI KAZE KOCHA SIMBA ATAJA SABABU ZA KUTOCHEZESHA BEKI MZIMBAMBWE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply