Simba SC

WAWA AWAFUNIKA CHAMA NA MIQUISSONE SUDANI

admin March 4, 2021 6:47 pm


SUDAN. PENGINE Dar es Salaam, wapenzi wa soka na hata wale ambao si mashabiki huenda wakawa wanalitaja zaidi jina la kiungo Clatous Chama kuliko beki Pascal Wawa.

Ukweli usiopingika katika ardhi ya Tanzania moja ya mastaa wa Simba ambao wanatajwa sana ni Chama na Luis Miquissone.

Kwa hapa Sudan hali ni tofauti mchezaji wa Simba ambaye jina lake linatajwa zaidi na mashabiki wa soka ni, Wawa.

Tangu msafara wa Simba, ilipofika uwanja wa ndege Wawa amekuwa akitajwa zaidi mpaka na wahudumu wa hapo na si Chama wala Miquissone.

Kuna baadhi ya watu wengine walishindwa kujizuia mpaka kuamua kupiga kelele za kumuita jina lake na wengine kumuomba picha.

Hali hiyo ya Wawa haikuishia hapo bali hata katika hoteli, akikatiza tu huitwa, katika uwanja wa mazoezi ma maeneo mengine.

“Hapa ni kama nyumbani nilicheza soka si chini ya miaka mitano tena kwa kiwango cha juu ndio maana nafahamika,” alisema.

“Hapa ni kama nyumbani watu wengi wananifahamu ndio maana wananiita na kuniomba picha.

” Naweza pia kuzungumza mpaka lugha yao  kwani nimecheza kwa muda mrefu kwa mafanikio na kiwango cha juu,” alisema Wawa.

ALICHOSEMA MANARA HUKO SUDAN BAADA YA YANGA SC KUFUNGWA LEO LIGI YA MABINGWA AFRIKA KWA WANAWAKE KUANZA KATI YA OKTOBA NA NOVEMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply